Yanga leo inaanza rasmi hamasa kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly ambao utapigwa Disemba 02 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Baada ya mchezo dhidi ya CR Belouizdad kesho, mchezo utakaofuata ni dhidi ya Al Ahly ukiwa ni mchezo wa kwanza nyumbani na mchezo wa pili katika makundi
Ni saa 5 asubuhi leo Alhamisi eneo ni Karume, Ilala mauzo ya tiketi kuelekea mchezo huo yatazinduliwa rasmi
Hamasa itazinduliwa kwa kushuhudia marudio ya mchezo dhidi ya Simba ambao Wananchi waliibuka na ushindi wa mabao 5-1 '5G' ambayo ilirejesha utulivu Dar
"Na kama kawaida yetu, hatuendi kinyonge , hamasa ya Shangwe la Mashabiki wa Yanga linaanza leo kwa waandamizi kutazama marudio ya Mnara ulivyosoma"
"Ndiooo .. Mtambo hauwezi kuhamia Kimataifa kimya Kimya . Saa 5:00 Asubuhi moto utawaka pale Karume Jijini Dar Es Salaam. Uwanja wa Mkapa ni Full House Dec 2 .Hakuna Stori Tofauti na hiyo.Ukichelewa kupata Tiketi yako usije kutulaumu Baadae," aliandika Kamwe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii