Msafara wa kwanza wa kikosi cha Yanga umeondoka nchini Alfajiri kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo ligi ya mabingwa dhidi ya CR Belouizdad utakaopigwa Ijumaa, Novemba 24
Yanga inakwenda Algeria ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya USM Alger mara ya mwisho walipokuwa nchini humo msimu uliopita katika mchezo wa fainali kombe la Shirikisho barani Afrika
Pamoja na changamoto ya ratiba, Wananchi wako imara na kazi itakuwa moja huko Algeria, kusaka alama tatu





ADVERTISE HERE