Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ya Dar es Salaam inatarajia kusikiliza usuluhishi katika kesi ya kiungo nyota wa Yanga, Jonas Mkude ambaye anaidai Kampuni ya Mohamed Enter-prises (Tanzania) Limited fidia ya Sh1 bilioni kwa kutumia picha yake katika matangazo ya biashara ya bidhaa zake bila ruhusa yake
Kesi hiyo ya madai namba 192 ya mwaka 2023 ilikuja mbele ya Jaji, Butamo Philip wa Mahakama hiyo leo Jumatatu, Novemba 20, 2023 kwa ajili ya kutajwa ambapo imepangwa kusikilizwa usuluhishi Novemba 27, 2023
Mbali ya kudai fidia hiyo Mkude ameiomba mahakama hiyo iamuru kampuni hiyo kumlipa mrabaha unaotokana na manufaa ambayo kampuni hiyo imeipata
Katika madai hayo Mkude aliilalamikia kampuni hiyo kutumia picha yake kutangaza biashara ya huduma zake na bidhaa kupitia mitandao ya kijamii ya Instagram, Facebook na Twitter ikijulikana kama X bila ya kupata ridhaa kutoka kwake