Jana Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Gerson Msigwa aliikabidhi timu ya Taifa ya Tanzania Tsh Milioni 10 ikiwa ni bonas ya Rais Samia Suluhu Hassan kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Niger
Msigwa alikabidhi fedha hizo baada ya timu kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikitokea Morocco
Aidha Msigwa alisema Rais Samia amenunua tiketi zote zilizokuwa zimebaki Mzunguuko hivyo mashabiki wataingia bure kuishangilia Stars katika mchezo dhidi ya Morocco hapo kesho
"Kama mnavyojua Mheshimiwa Rais aliahidi kwamba kwenye safari ya taifa stars kila goli atakuwa anatoa Sh milion 10. Fedha hizi ninakabidhi kutimiza ahadi ya Rais"
"Lakini pia Rais Samia amelipia eneo la mzunguko lenye takriban viti 30,000 kwajili ya Watanzania watakao fika kuishangilia timu ya taifa siku ya Jumanne Novemba 21 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa ikiwa ni sehemu ya kampeni maalum iitwayo 'oparesheni Samia Kombe la Dunia' kwajili ya kuhamasisha timu Kushiriki kombe la dunia," alisema Msigwa
Mchezo dhidi ya Morocco utapigwa Jumanne Nov 21 uwanja wa Benjamin Mkapa, saa 4 usiku