Skudu aitamani CR Belouizdad

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Nov 2023
Skudu aitamani CR Belouizdad

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mahlatse Makudubela ‘Skudu’ amesema baada ya kupona majeraha yuko tayari kutumika kikamilifu pale atakapohitajika na benchi la ufundi

Skudu aliyesajiliwa msimu huu kutoka Marumo Gallants ya Afrika Kusini, amerejea uwanjani hivi karibuni na kupewa dakika chache kwenye baadhi ya mechi ikiwamo mechi dhidi ya Simba iliyomalizika kwa Wananchi kuibuka na ushindi wa mabao 5-1

Skudu amesema baada ya kupona ni suala la kuaminiwa na kupewa muda wa kutosha ndani ya uwanja ili kuthibitisha usajili wake, akilenga mchezo ujao wa makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CR Belouizdad

Yanga inatarajiwa kushuka uwanjani ikiwa ugenini Algeria kuvaana na CR Belouizdad Ijumaa ya wiki ijayo na Skudu amesema kwa sasa yuko tayari kwa ajili ya mchezo huo

"Niko fiti sana, ninachosubiri benchi la ufundi linipe muda wa kutosha uwanjani. Nakiamini kikosi chetu na tupo tayari kwa mechi hii. Tuna timu iliyokamilika vizuri na tutakachojaribu kufanya ni kurudia mafanikio yetu ya msimu uliopita"

"Mwanzo mzuri umeonekana kwa mechi zetu za awali kwenye Ligi ya Mabingwa. Msimu uliopita tulicheza fainali Kombe la Shirikisho, malengo ni makubwa msimu huu," alisema Skudu

Yanga imekuwa kwenye kiwango bora, ikishinda mechi nane kati ya tisa ilizocheza za Ligi Kuu Bara, ikipoteza moja dhidi ya Ihefu huku ikifunga mabao 26 na kufungwa matano na kuvuna jumla ya pointi 24

Skudu akicheza mechi tatu akitumia jumla ya dakika 76, zikiwamo 57 za Ihefu, dakika 18 za Singida Fountain Gate na dakika nne za mechi ya Simba na Yanga

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’