Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema wanatambua mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya CR Belouizdad utakuwa mgumu kwa kuwa wapinzani wao pia wana timu nzuri
Hata hivyo Kamwe amesema wana imani na ubora wa kikosi walichonacho pamoja na benchi la ufundi chini ya kocha Miguel Gamondi
Novemba 24 Yanga itakuwa ugenini huko Algeria kuwakabili mabingwa wenzao CR Belouizdad Wananchi watahitaji ushindi au hata alama moja
"Kila kitu kinaenda vizuri kuelekea mchezo wetu huo dhidi ya CR Belouizdad, benchi la ufundi linaendelea kukisuka kikosi kwenda kutafuta matokeo mazuri ugenini"
"Licha ya wachezaji kutokamilika wote, wengine wakiwa kwenye majukumu ya timu za Taifa, lakini Kocha (Gamondi) anaendelea kuwaweka imara nyota waliopo kambini"
"Ukiangalia rekodi za msimu uliopita mashindano ya kimataifa ugenini tumefanya vizuri, msimu huu tunataka kuanzia tulipoishia," alisema Kamwe.