Kikosi cha Yanga chini ya Kocha Miguel Gamondi kinaendelea kujifua Avic Town kujiandaa na mchezo wa kwanza kundi D ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria
Gamondi anaweka mikakati yake sawa kuhakikisha kikosi chake kinaendeleza ubabe wake katika mechi za ugenini kwenye mashindano ya CAF
Tangu msimu uliopita katika mashindano ya CAF, Yanga imeshinda mechi sita mfululizo ugenini
Wananchi walianza na TP Mazembe (1-0), Rivers United (2-0), Marumo Gallants (2-1), USM Alger (1-0), ASAS Fc (2-0) na Al Merrikh (2-0)
Hii ni rekodi kwa Yanga kushinda ugenini mfululizo, Gamondi amepania kuendeleza rekodi hiyo akiwa tayari ameiongoza Yanga kushinda mechi zote za hatua ya awali na kuipeleka makundi baada ya miaka 25







ADVERTISE HERE