Yanga imejichimbia Avic Town ikiendelea na maandalizi ya mchezo wa kwanza wa kundi D ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Novemba 24 huko Algeria katika uwanja uleule ambao Yanga iliigaragaza USM Alger kwenye mchezo wa pili wa fainali ya kombe la Shirikisho msimu uliopita
Gamondi amewahi kuinoa CR Belouizdad hivyo hatakuwa mgeni huko Algeria. Mikakati yake ya kushinda mchezo huo aliianza mapema ambapo taarifa za kuaminika ni kuwa mchambuzi wa video (video analyst) wa Klabu ya Yanga, Khalil Ben Youssef alishawasili nchini Algeria wiki mbili zilizopita
Jana alishuhudia mchezo wa ligi kuu ambao CR Belouizdad walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Paradou
Belouizdad watacheza mechi nyingine ya Ligi Novemba 19 kabla ya mchezo dhidi ya Yanga utakaopigwa Novemba 24 saa 4 usiku
Kikosi cha Gamondi nacho kinatarajiwa kucheza mechi moja ya kirafiki mwishoni mwa wiki kabla ya safari ya Algeria