Hiki kinaweza kuwa kipindi kigumu zaidi kwa mashabiki wa Simba kutokana na kero wanazokumbana nazo kutoka kwa watani zao Yanga
Ni baada ya kipigo cha kihistoria cha mabao 5-1 ambacho Simba walikumbana nacho kutoka kwa Yanga pale uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga imeendelea kusimika mabango ya 5G katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam kwa ajili ya kuweka kumbukumbu ya kipigo hicho
Yanga na Simba zina historia ya aina yake pale yanapokuja masuala ya utani, huu ni utamaduni ambao uko kwa miaka mingi, kinachofanyika sasa ni kuendeleza tu
Mwaka 2012 Yanga ilipoteza dhidi ya Simba kwa kufungwa mabao 5-0, ilikuwa miaka 11 migumu kwa mashabiki wa Yanga kwani ni kipigo ambacho watani zao Simba walikitumia kuwakejeli kila wakati
Sasa shilingi imegeuka upande wa pili, ni zamu yao kuvumilia 'kero' za Wananchi, minara hii ya 5G itatapakaa kila kona ya jiji la Dar es salaam na hata mikoani...!Β
