Mbunifu wa jezi za Yanga Sheria Ngowi tayari amefanya kazi yake ya kuandaa jezi zenye hadhi ya Kimataifa ambazo Yanga watazitumia kuanzia hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika
Tukio kubwa la utambulisho wa jezi hizo litajiri wakati wowote, kuanzia leo
Ngowi amesema jezi ya Kimataifa ya msimu huu itakuwa bora zaidi ya zile zilizotumika kwenye michuano ya kombe la Shirikisho msimu uliopita
Chini ya ubunifu wa Ngowi, Yanga haijawahi 'kufeli' kwenye jezi, bila shaka utaratibu huo utaendelea katika jezi mpya zinazosubiriwa na Wananchi kwa hamu kubwa
ADVERTISE HERE