Yanga yaanza maandalizi ya kuikabili CR Belouizdad

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Nov 2023
Yanga yaanza maandalizi ya kuikabili CR Belouizdad

Baada ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki, kikosi cha Yanga kimerejea mazoezini kujiandaa na mikiki mikiki ya hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika

Wananchi ambao wako kundi D, wataanzia ugenini Novemba 24 nchini Algeria katika mchezo dhidi ya CR Belouizdad

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema leo wachezaji wamefanya 'session' moja ya mazoezi Avic Town

Hata hivyo Kamwe amesema ipo changamoto inayotokana na idadi kubwa ya wachezaji kwenda kwenye majukumu ya timu za Taifa

"Tumeanza mazoezi Avic Town, leo tulikuwa na session moja ya mazoezi yakisimamiwa na kocha Miguel Gamondi na benchi la ufundi kwa ujumla"

"Tuna changamoto ya ratiba kwani wachezaji wengi wako kwenye majukumu ya timu za Taifa na pengine wengine tutaungana nao nchini Algeria"

"Mchezo wa mwisho wa kuwania kufuzu kombe la Dunia ni Novemba 21 na mchezo wetu dhidi ya CR Belouizdad utapigwa Novemba 24," alisema Kamwe

Wachezaji 11 wameondoka kwenda majukumu ya timu za Taifa ambapo nyota nane wako timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' huku Khalid Aucho akijiunga na Uganda, Stephane Aziz Ki (Burkina Faso) na Djigui Diarra (Mali)

Nyota walio kikosi cha Stars ni Aboutwalib Mshery, Metacha Mnata, Nickon Kibabage, Dickon Job, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Mudathir Yahya na Clement Mzize

Kikosi cha Gamondi kilichobaki hakina golikipa kwani makipa wote wameenda kwenye majukumu ya timu za Taifa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’