Gamondi akabidhi mapendekezo ya usajili dirisha dogo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Nov 2023
Gamondi akabidhi mapendekezo ya usajili dirisha dogo

Wakati mashabiki wa Yanga wakiendelea kutamba mtaani kutokana na kiwango bora kilichoonyeshwa na timu hiyo iliyoshinda mechi nane kati ya tisa za Ligi Kuu na kuwa vinara wa kutupia mipira kambani, kocha mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi anapiga hesabu za kuimarisha kikosi chake zaidi

Yanga inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 24 na mabao 26, kwa sasa inajiandaa kwa ajili ya mechi sita za makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikitarajiwa kuanza ugenini dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria, Novemba 24 kabla ya kuikaribisha Al Ahly ya Misri moja baadae jijini Dar es Salaam.

Lakini pamoja na kuwa kwenye maandalizi kwa ajili ya mechi hizo dhidi ya klabu kutoka Afrika Kaskazini, imeelezwa kuwa kocha Gamondi tayari ameshawasilisha ripoti ya benchi la ufundi kwa mabosi wa klabu hiyo, ambayo imeanza kufanyiwa kabla hata kabla dirisha la usajili halijafunguliwa Desemba 16.

Taarifa kutoka ndani ya Yanga ni ripoti ya Gamondi ambayo imeshaanza kufanyiwa kazi na mabosi wawili wa juu wa klabu hiyo

Kulingana na Mwanaspoti, ripoti hiyo imeonyesha mchezajai wa kwanza anayetakiwa ni mshambuliaji mwenye ubora mkubwa wa kufunga atakayekuja kuongeza makali ya eneo la ushambuliaji la mabingwa hao, kwani kwa sasa hajaridishwa na kazi, licha ya timu hiyo kuongoza kwa kufunga mabao mengi katika Ligi Kuu.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kuna uwezekano mkubwa straika wa sasa Hafiz Konkoni kupewa mkono wa kwaheri endapo Yanga itapata nyota wanayemfukuzia kwa sasa ambaye hata hivyo jina lake limefanywa siri.

Gamondi ametaja pia kuhitaji winga mwenye kasi na kujua kupangua ukuta ambaye naye akitakiwa kuwazidi mawinga wote waliopo kikosini akiwamo Mahlatse Makudubela β€˜Skudu’, Maxi Nzengeli, Jesus Moloko na Denis Nkane.

Eneo la kiungo mkabaji linatajwa kuwa sehemu ya mapendekezo hayo, kwa ajili ya kuongeza nguvu eneo hilo ambalo kwa sasa Khalid Aucho ndiye tegemeo

Tayari Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ameanza kufanyia kazi mapendekezo hayo jana kupitia Mawasiliano ya simu na Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe, akiwaahidi wapenzi na wanachama wa Yanga kuwa watakamilisha usajili wa dirisha dogo mapema na Yanga itakuwa klabu ya kwanza kutambulisha wachezaji wapya pale dirisha litakapofunguliwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
29m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’