Kocha wa zamani wa Yanga Nasreddine Nabi amepata msiba wa kufiwa na Baba yake mzazi huko Tunisia
Nabi aliyefanya kazi kubwa kuirejesha heshima ya Yanga kwenye soka la ndani na Kimataifa, leo alipaswa kuiongoza timu yake ya AS FAR katika mchezo wa ligi lakini amrejea Tunisia
Msemaji wa zamani wa Yanga Haji Manara amethibitisha taarifa za msiba huo uliotokea leo
"Nimepokea Taarifa sasa hivi Kocha wetu zamani wa Yanga Professor Nasredine Nabi amefiwa na Baba yake Mzazi huko Monastir nchini Tunisia Asubuhi ya leo.
Nimeongea na Kocha Nabi Mchana huu pamoja na Bernard Morrison kunipa taarifa hizi ili niwajulishe Watanzania na Washabiki wetu ambao walikaa na Kocha Nabi vzuri mno!
Kwa leo Nabi hatakaa jukwaani team yake itakapokuwa ikicheza mechi ya ligi na tayari maandalizi ya kwenda kwao Tunisia kuwahi msiba yanaendelea.
Kwa niaba yenu nimempa pole nyingi Kocha wetu ambae amejawa na huzuni ya kumpoteza Baba yake
Wananchi tunampa pole profesa Nabi Mwenye ez Mungu ampe uvumilivu katika kipindi hiki kigumu..