Kama mna ushahidi wa rushwa nendeni TAKUKURU - Simon

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Nov 2023
Kama mna ushahidi wa rushwa nendeni TAKUKURU - Simon

Mkurugenzi wa Sheria wa klabu ya Yanga Simon Patrick ameunga mkono kauli iliyotolewa Bungeni leo na Mhe. George Simbachawene, Waziri Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora kuwa kama klabu ya Simba ina ushahidi wa baadhi ya wachezaji wake kuhongwa na kupelekea kipigo cha mabao 5-1 kutoka kwa Yanga, basi ni vyema wakapeleka malalamiko hayo ofisi za TAKUKURU

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Simon ameandika ujumbe huu;

"Kwa mujibu wa kifungu na. 15 cha sheria na. 329, kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022, kinasema kutoa na kupokea rushwa ni kosa la jinai na adhabu yake ni faini pamoja na kifungo kuanzia miaka 3 mpaka 5.

Kama mnahisi kuna wachezaji au viongozi walipokea rusha, ni vyema kufuata ushauri wa Mh. Simbachawene leo Bungeni kwenda ofisi za TAKUKURU - Temeke kufungua kesi, kisha kuiandikia TFF na FIFA ili hatua kali zichukuliwe kwa maendeleo ya mpira wetu.

Lakini kumbukeni, kumtuhumu mtu kwa kosa kubwa kama hilo bila ushahidi adhabu yake unaweza kuishia kulipa mabilioni ya fedha kwa reputation damage.

Ushauri wa bure, nendeni mkafungue kesi kama mna ushahidi, kinyume na hapo jipangeni upya mpira ni mchezo wa wazi, nyie sio timu ya kwanza kupigwa 5G msimu huu.

Haiwezekani wachezaji wa kuteka Airport waje wapambane na wachezaji waliofanyiwa scouting!"

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’