Msako wa alama tatu unaendelea Mkwakwani leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 Nov 2023
Msako wa alama tatu unaendelea Mkwakwani leo

Kikosi cha Yanga kiko mkoani Tanga ambapo leo saa 12:30 jioni watashuka uwanja wa Mkwakwani kumenyana na Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu ya NBC

Baada ya ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya watani zao Simba kwenye mchezo uliopita, Yanga ina nafasi ya kuzidi kuchimbia kileleni mwa msimamo wa ligi leo kama itaibuka na ushindi

Hata hivyo hautakuwa mchezo mwepesi kwani Coastal Union haijawahi kuwa timu rahisi inapocheza na Yanga katika uwanja wa Mkwakwani

Katika Mkutano na Wanahabari jana, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi alisema vijana wake wako tayari kwa mchezo huo ambao wanatarajia utakuwa mgumu

Gamondi alisema licha ya Coastal Union kuwa na mwendo wa kusuasua msimu huu, lakini anafahamu leo watahamasika zaidi kwa kuwa wanacheza na Yanga

Gamondi alidokeza kikosi chake kitakuwa na mabadiliko machache, kuna wachezaji walipata majeraha kwenye mchezo uliopita dhidi ya Simba

Yanga ilitua mkoani Tanga juzi usiku na jana jioni wachezaji walipata nafasi ya kufanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Mkwakwani tayari kwa mchezo huo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
6h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
14h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’