Stars kuikabili DR Congo leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Mar 2018
Stars kuikabili DR Congo leo
Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inacheza mchezo wake wa pili wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Jamhuri ya Demokrasia Congo leo Jumanne Machi 27, 2018, kwenye uwanja wa Taifa.

Huu ni mchezo muhimu katika tarehe zilizopo kwenye kalenda ya FIFA ambapo kocha msaidizi

Hemed Morocco tayari amesema wanauchukulia kwa uzito mkubwa na nia ni kufanya vizuri.

Katika mwezi huu wa Machi, Taifa Stars inacheza mechi mbili za kirafiki. Mechi ya kwanza ikiwa tayari imechezwa nchini Algeria dhidi ya Timu ya Taifa ya nchi hiyo.

Kikosi hicho cha Taifa Stars kitaongozwa na nahodha wake Mbwana Samatta anayecheza katika timu ya KRC Genk ya Ubelgiji.

Mbali na Samatta, wachezaji wengine walioitwa kwenye kikosi na kocha Salum Mayanga ni pamoja na Aishi Manula, Ramadhan Kabwili, Mohamed Abdulrahman, Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Abdi Banda, Kelvin Yondan, Himid Mao Simon Msuva, Mudathir Yahya, Mbwana Samatta, Said Ndemla na Shiza Kichuya.

Wengine ni Hassan Kessy, Erasto Nyoni, Shaban Chilunda, Ibrahim Ajib, Yahaya Zayd, Mohamed Issa, Rashid Mandawa na Faisal Salum.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’