Kituo kinachofuata ni Mkwakwani Tanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
6 Nov 2023
Kituo kinachofuata ni Mkwakwani Tanga

Baada ya kukata ngebe za watani hapo jana kwa ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Simba katika mchezo wa ligi kuu ya NBC, Yanga haina muda wa kupoteza kwani inaelekeza nguvu katika mchezo unaofuata

Keshokutwa Jumatano, Novemba 08 katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga, Yanga itakuwa mgeni wa Coastal Union katika mchezo wa ligi kuu raundi ya tisa

Ni ratiba yenye changamoto kwa Wananchi hasa ikizingatiwa wamecheza jana mechi ngumu na watahitaji kusafiri kuelekea Tanga kwa ajili ya mchezo huo

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesisitiza kuwa wanahitaji kuendeleza mwenendo wa ushindi katika kila mechi ili kuhakikisha wanakuwa kwenye nafasi nzuri ya kutimiza malengo ya kutetea ubingwa kwa msimu wa tatu mfululizo

Baada ya mchezo huo Yanga itarejea Dar kujiandaa na mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya CR Belouizdad utakaopigwa Novemba 25 huko Algeria

Ligi inatarajiwa kusimama baada ya mechi za raundi ya tisa kupisha kalenda ya FIFA

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’