Simba imekuwa timu ya tatu kwenye ligi kuu ya NBC msimu huu kupokea kipigo cha 5G kutoka kwa Yanga
Ni timu ya nne kufungwa mabao matano na Yanga katika mashindano yote
Mnara wa 5G ulianza kusoma katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC, ukasoma tena kwenye mchezo wa mkondo wa pili hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya ASAS FC
JKT Tanzania nao wakaingia kwenye mfumo, wakala 5G pale uwanja wa Azam Complex ukiwa ni mchezo wa ligi kuu
Mnara wa 5G ukapoa kwa muda na jana umesoma tena, safari hii ni uwanja wa Benjamin Mkapa, Simba wakiingia kwenye mfumo na kupata zawad yao!
Ni wazi kwa jinsi kikosi cha kocha Miguel Gamondi kinavyocheza, hizi 5G zitaendelea hazijaisha kuna timu inaweza kukumbana na dhahma kubwa zaidi
Ni mechi nane tu mpaka sasa Yanga imecheza kwenye ligi, bado mechi nyingine 22!