Ndio! pengine sasa heshima kwa mafanikio waliyopata Yanga katika misimu hii miwili itakaa mahali pake
Wakati Yanga ikitajwa kuwa miongoni mwa timu 10 bora barani Afrika ikiwania tuzo ya klabu bora ya mwaka, walibeza sana
Msimu uliopita Yanga ilicheza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika ikashinda ugenini dhidi ya USM Alger lakini bado walioponda wakidai Yanga imekutana na vibonde
Kipigo hichi cha mabao 5-1 ambacho Simba wamekutana nacho, kitawakumbusha daraja la Yanga ambao wako sasa
Sio kwa bahati mbaya Yanga kupata mafanikio hayo Kimataifa pamoja na kutwaa mataji yote ya ndani katika misimu miwili iliyopita
Simba leo wamekutana na Yanga ambayo siku zote wamedai inafunga vibonde, itoshe kusema nao wamekuwa vibonde wa Yanga!
Daraja la kina Maxi Nzengeli, Pacome Zouzoua, Stephane Aziz Ki, Mudathir Yahya, Khalid Aucho na nyota wengine wa Yanga ni la juu sana
Uongozi wa Yanga chini ya Rais Injinia Hersi Said wanastahili pongezi kwa usajili makini waliofanya msimu huu
Huu unaweza kuwa msimu mwingine wa furaha kwa Wananchi. Leo wamesema...!