FT : Simba 1-5 Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Nov 2023
FT : Simba 1-5 Yanga

Rekodi imeandikwa uwanja wa Benjamin Mkapa leo 5G ikirejea tena  mitaa ya Twiga na Jangwani

Ulichoona hapo juu hujakosea! Yanga imeibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Simba

Ilikuwa suala la muda tu, ubora wa Yanga ukadhihiri kwenye kipindi cha pili Wananchi wakifunga mabao manne baada ya sare ya 1-1 mpaka wakati wa mapumziko

Kennedy Musonda aliitanguliza Yanga kwa bao safi la kichwa kwenye dakika ya tatu akimalizia krosi ya Yao Kouassi

Simba walirejesha bao hilo dakika chache baadae kwa mpira wa kichwa kutoka kwa Kibu Denis

Lakini shughuli waliyokutana nayo kwenye kipindi cha pili kwa hakika hawatakuja kusahau maisha mwao

Maxi Nzengeli aliweka kambani bao la pili baada ya pasi ya Aziz Ki kabla ya Aziz Ki kufunga la tatu akipokea pasi ya Clement Mzize aliyengia kwenye kipindi cha pili na kubadili taswira ya mchezo

Alikuwa Mzize tena aliyetengeneza bao la nne lililofungwa na Nzengeli kabla ya Pacome Zouzoua kufunga la tano baada ya Nzengeli kuangushwa kwenye eneo la hatari

Leo ni siku ya furaha kwa Wananchi, zile tano walizokuwa wakitamba nao hatimaye zimelipwa....!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
29m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
23h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’