Kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Oktoba 2023 Ligi Kuu ya NBC
Aziz Ki ameshinda tuzo hiyo baada ya kufunga mabao manne katika mechi za ligi kuu walizocheza Yanga mwezi Oktoba
Ki alichuana na Maxi Nzengeli na Moses Phiri wa Simba
Ni tuzo ya pili kwa Aziz Ki kwa mwezi Oktoba akiwa pia mchezaji bora wa Yanga katika mwezi huo
Ki alishinda tuzo ya Yanga mbele ya Nzengeli na Dickson Job
Kwa hakika huu ni msimu wa 'matuzo' kwake
ADVERTISE HERE