Mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra ameingia katika kinyan'ganyiro cha kuwania tuzo ya golikipa bora wa mwaka barani Afrika katika tuzo za CAF zitakazotolewa Disemba 11 huko Morocco
Diarra yuko kwenye nafasi nzuri ya kushinda tuzo hiyo kutokana na kiwango bora alichoonyesha katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika msimu uliopita
Miongoni mwa walinda lango anaochuana nao ni Andre Onana wa Manchester United (Cameroon), Mohammed Alshenawy wa Al Ahly, Edawrd Mendy wa Senegal (msimu uliopita aliitumikia Chelsea Fc) na wengine
Diarra pia ametajwa kuwania tuzo ya mchezaji bora wa mashindano ya ndani ya CAF katika tuzo hiyo pia akitajwa Fiston Mayele ambaye kwa sasa yuko Pyramids ya Misri

ADVERTISE HERE