Pengine Jumapili kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua atapata nafasi ya kutumika ipasavyo katika mchezo wa derby ya Kariakoo dhidi ya Simba ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Pacome alitumika kwa takribani dakika 10 kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii uliopigwa jijini Tanga katika uwanja wa Mkwakwani
Nyota huyo kutoka Ivory Coast ameanza vyema maisha yake katika klabu ya Yanga, akiwa amefunga mabao matatu na kutoa pasi moja ya bao katika ligi kuu ya NBC
Habari njema kwa Wananchi ni kuwa Pacome amerejea mazoezini baada ya mapumziko kutokana na majeraha aliyopata katika mchezo dhidi ya Singida BS
Pacome na Stephane Aziz Ki walipata majeraha madogo katika mchezo huo lakini bila shaka wote watakuwa tayari kuikabili Simba siku ya Jumapili
ADVERTISE HERE