Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Mbwana Samatta amewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu yao ya Taifa itakapokuwa inacheza na DR Congo keshokutwa.
Stars inatarajiwa kuikabili DR Congo kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya FIFA. Mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Taifa, Jumanne, March 27 2018.
Samatta amesema wamejipanga kuhakikisha wanaibuka na ushindi katika mchezo huo baada ya kufungwa kwa mabao 4-1 kwenye mchezo uliuopita dhidi ya Algeria.
Amewataka mashabiki kutochoka kuishangilia timu yao licha ya kipigo hicho kutoka kwa vigogo hao wa soka barani Afrika.
"Ni kweli matokeo siyo mazuri kwetu ingawa lengo letu lilikuwa ushindi lakini Watanzania hawapaswi kukata tamaa kwa sababu Algeria ni moja ya timu kubwa Afrika.
"Kitu cha msingi waendelee kutusapoti kwani tunaimarisha timu kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye michuano ya kufuzu fainali ya Mataifa ya Afrika,Γ’β¬Β amesema Samatta.
Stars inaendelea na maandalizi kwenye uwanja wa Taifa kuelekea mchezo dhidi ya DR Congo chini ya kocha Mkuu Salum Mayanga.

ADVERTISE HERE