Wakati upande wa pili wakitamba kuelekea mchezo wa dabi ya Kariakoo kati ya Simba dhidi ya Yanga, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi hana wasiwasi wowote kuelekea mchezo huo
Jana Afisa habari wa Simba Ahmed Ally alitumia Mkutano wake na wanahabari kumkebehi Gamondi baada ya kuhudhuria mechi za Simba zilizopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa akimtaka ahudhurie na mazoezi ya timu hiyo Bunju
Gamondi ameweka mkakati wa kushinda mchezo huo ili kuhakikisha Yanga inabaki kileleni mwa msimamo wa ligi
"Tucheze kama tuko mazoezini hili ni jambo muhimu sana, tusisahau," Gamondi aliweka ujumbe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Jana Yanga ilianza rasmi maandalizi kuelekea mchezo huo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali
Habari njema ni kuwa Gamondi tayari amefahamu namna gani timu yake itacheza mchezo huo muhimu ili kushinda
Utakuwa mchezo wa pili baina yake na kocha wa Simba Robertinho Oliveira aliyeibuka mshindi kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii kupitia mikwaju ya penati baada ya suluhu ya bila kufungana
Pengine Gamondi alistahili kushinda mchezo huo kwani Yanga ilitawala tangu dakika ya kwanza yalikosekana mabao tu
Wakati anakwenda kuikabili Simba siku ya Jumapili, wakati huu ana silaha za kutengeneza na kufunga mabao
Stephane Aziz Ki kinara akiwa na mabao sita, Maxi Nzengeli mabao matano, Pacome Zouzoua mabao matatu huku Yao Kouassi akiwa na assist nne