Yanga kurejea mazoezini kesho, kuwakosa walio Stars

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Mar 2018
Yanga kurejea mazoezini kesho, kuwakosa walio Stars
Kikosi cha Yanga kinaendelea na mazoezi kesho Jumatatu baada ya mapumziko ya siku kadhaa ikiwa ni maandalizi kuelekea mchezo wa kombe la FA dhidi ya Singida United utakaopigwa kwenye uwanja wa Namfua April 01.

Baadhi ya wachezaji walio na majukumu na kikosi cha timu ya Taifa ambao ni Ramadhani Kabwili, Hassani Kessy, Gadiel Michael, Kelvin Yondani na Ibrahim Ajib wataendelea kukosekana hadi baada ya mchezo wa Stars dhidi ya DR Congo.

Stars itacheza na DR Congo keshokutwa Jumanne March 27 katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki ulio kwenye kalenda ya FIFA utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Habari njema kwa kikosi cha Yanga ni kwamba sasa hakuna majeruhi wachezaji wote wakiwemo Amissi Tambwe, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma na Yohana Nkomola wamerejea kikamilifu kujifua na wenzao baada ya kumaliza program binafsi za mazoezi.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
23h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’