Yanga imejiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida BS katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Mabao ya Maxi Nzengeli yaliihakikishia Yanga kuondoka na alama zote tatu na kufikisha alama 18 alama tatu zaidi juu ya msimamo wa ligi
Wananchi walihitaji dakika 45 za kipindi cha kwanza kumaliza mchezo huo kwa mabao mawili ya Maxi aliyefunga dakika za 30 na 39
Kipindi cha pili Yanga ilitengeneza nafasi nyingi zaidi pengine ilistahili kuondoka na ushindi mnono lakini nafasi hazikutumika ipasavyo
Ni wazi vijana wa Gamondi leo walikuwa na 'fartique' kwani hawakuwa katika ile kasi iliyozoeleka
Pengine ni kutokana na mchezo dhidi ya Azam Fc ambao wachezaji walimwagika jasho jingi kupata ushindi, leo zilihitajika alama tatu zaidi
Max amesogea mpaka nafasi ya pili katika orodha ya vinara wa ufungaji bora akifikisha mabao matano sawa na Jean Baleke wa Simba
Stephane Aziz Ki anaendelea kubaki juu akiwa amepachika mabao sita


