Aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars, ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa, amesema kutokuwa na msingi bora wa vilabu hapa nchini, ndiyo chanzo cha kutokuwa na timu bora ya taifa.
Mkwasa ameyasema hayo alipotembelewa na Azam TV ofisini kwake, ambapo amesema kuwa moja ya jambo linaloifanya Taifa Stars kushindwa kuhimili mechi ngumu ni kukosa wachezaji wenye uwezo wa kuusoma mchezo kwa haraka na wanashindwa kuchukua maamuzi kwa uwezo binafsi kwa maslahi ya timu, na badala yake wanategemea maelekezo zaidi.
Kauli hiyo inakuja kufuatia Taifa Stars kupoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Algeria uliopigwa Machi 22 mwaka huu nchini Algeria, ambapo ilifungwa mabao 4-1, na sasa ikiwa inajiandaa kwaajili ya mchezo mwingine dhidi ya DRC, utakaopigwa Machi 27 jijini Dar es Salaam.
Mkwasa alikuwa akitoa tathmini yake juu ya mchezo huo, ikiwa imepita miaka miwili tangu timu hiyo ichapwe 7-0, wakati yeye akiwa kocha wa timu hiyo.

ADVERTISE HERE