Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma amewatoa hofu mashabiki kuwa sasa amepona kabisa majeraha yake na Jumanne ataanza rasmi mazoezi.
Msimu uliopita haukuwa mzuri sana kwa Ngoma ambaye aliisaidia Yanga kwenye mzunguuko wa kwanza wa VPL pekee kwa kufunga mabao nane.
Lakini sasa ameeleza kuwa anafahamu ana deni kubwa kwa Yanga na ameahidi kuisaidia Yanga kutwaa taji la nne mfululizo la VPL pamoja na kuhakikisha Yanga inatinga hatua ya makundi, ligi ya mabingwa barani Afrika.
Ngoma alikuwa nje ya uwanja kwa miezi minne akitibiwa nchini Afrika Kusini matatizo ya goti lililomsumbua sana msimu uliopita.
Madaktari waliokuwa wakimtibu wameihakikishia Yanga kuwa Ngoma amepona kwa asilimia 100 na anaweza kuanza mazoezi sasa.
Hakika Yanga itaendelea kuwa moto wa kuotea mbali msimu ujao licha ya wachezaji kadhaa kuondoka.
Safu ya ushambuliaji atakosekana Msuva ambaye hata hivyo namba yake itazibwa vizuri tu na wachezaji waliopo.
Aidha hata Niyonzima hajaacha pengo Yanga kwani Kamusoko anaweza kucheza namba yake kwa ufasaha zaidi. Safu ya ushambuliaji itakayoongozwa na Ngoma itaendelea kulishwa mipira na fundi huyu.

ADVERTISE HERE