Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema vijana wake wako tayari kuwapa burudani mashabiki wao katika mchezo wa ligi kuu ya NBC dhidi ya Singida BS ambao utapigwa kesho Ijumaa katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo kuelekea mchezo huo, Gamondi amesema anatambua hautakuwa mchezo mwepesi kwani Singida BS ina mabadiliko makubwa hasa baada ya ujio wa benchi jipya la ufundi
Hata hivyo Gamondi amesema watapambana ili kuhakikisha wanashinda mchezo huo na kuwapa furaha mashabiki wao ambao nyakati zote wamekuwa sambamba na timu yao
"Kesho tunakwenda kwenye mchezo mwingine mgumu dhidi ya Singida BS lakini malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo na kuwapa burudani mashabiki wetu wanaokuja kutupa nguvu kipindi chote cha mechi zetu tukiwa Uwanjani"
"Hautakuwa mchezo rahisi kwasababu kuna vitu vingi vimebadilika kwa mpinzani wetu Singida, wana benchi la ufundi jipya na lenye maarifa tofauti"
"Tutacheza kwa kujituma na kwa tahadhari kwasababu tunahitaji ushindi kwenye kila mchezo"
"Kwa kipekee kabisa napenda kuwashukuru mashabiki wetu kwa kutushangilia kwa nguvu na kutusaidia kupata ushindi dhidi ya Azam Fc kwa kutokea nyuma na nina imani kesho watajitokeza kwa wingi kwenye mchezo wetu dhidi ya Singida BS," alisema Gamondi