Kocha Mkuu wa timu ya vijana ya Yanga U20 Vicent Barnabas leo ameanza kwa sare ya mabao 2-2 ligi kuu ya Vijana U20 katika mchezo dhidi ya KMC
Mapema leo Yanga ilimtangaza Barnabas kuwa kocha mkuu wa kikosi hicho cha vijana
Barnabas aliyewahi kuwa winga kunako klabu ya Yanga, amewahi kuwika na kikosi cha vijana cha Mtibwa Sugar ambao ndio wababe wa soka la vijana kwa misimu minne iliyopita
Ligi Kuu ya Vijana U20 imeanza kutimua vumbi leo Yanga U20 ikiwa kundi A
Mchezo unaofuata utapigwa Oktoba 26 dhidi ya Simba U20


ADVERTISE HERE