Mpiga picha wa Yanga Sc, Frank Mpelumbe amepata uteuzi wa kuwa mpiga picha wa meza kuu katika mechi ya leo ya African Football League inayopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Mpembule amepewa majukumu hayo ya Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) ambapo atapiga picha za CAF kwenye eneo ambalo litakuwa na uongozi wa juu wa Shirikisho la soka Duniani (FIFA)
Rais wa FIFA Gianni Infantino ni miongoni mwa wageni mashuhuri wanaohudhuria hafla ya uzinduzi wa mashindano ya AFL
Mwamuzi mstaafu Pierluigi Colina, mkufunzi wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger na Rais wa CAF Patrice Motsepe nao watakuwepo
Mpembule amejitangaza kwa ubora wa kazi yake katika klabu ya Yanga kwani yeye ndio mpiga picha za Yanga zinazoonekana katika ubora wa kipekee kwenye kurasa za mitandao ya kijamii