Wachezaji Djigui Diarra, Stephane Aziz Ki na Khalid Aucho wanatarajiwa kuwasili leo kuungana na wenzao kwenye maandalizi ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc
Mchezo huo utapigwa Jumapili, Oktoba 22 katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema wachezaji hao wamechelewa kurejea nchini kutokana na majukumu ya timu za Taifa
"Diarra, Aucho na Aziz Ki wamechelewa kwa sababu timu zao za Taifa zilikuwa na mechi Oktoba 17. Leo tunatarajia wote watawasili na kuungana na wenzao kwenye maandalizi ya mchezo dhidi ya Azam Fc"
"Wachezaji wote waliokuwa na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' wamesharudi na tayari wako na timu Avic Town kujiandaa na mchezo huo," alisema Kamwe
Aidha Kamwe amewataka mashabiki wa Yanga kununua tiketi zao mapema na kujitokeza kwa wingi uwanja wa Azam Complex katika mchezo ambao wanahitaji ushindi
"Mashabiki wote wa Yanga sehemu ya kukutana Jumapili ni Azam Complex. Mchezo dhidi ya Azam Fc ni muhimu sana kwetu kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri"
"Tunafahamu Azam Fc msimu huu wanautaka ubingwa sasa kupata ushindi dhidi ya mwenzako unayewania nae ubingwa ni faida kubwa kwetu"