Huko Yanga unaambiwa kuna MAP, ramani inayobeba ushindi katika mechi ambazo Wananchi wanashuka uwanjani
MAP ni kifupisho cha majina ya nyota watatu Maxi Nzengeli, Aziz Ki na Pacome Zouzoua
Kama Fc Barcelona ilivyowahi kuwa na MSN (Messi, Suarez na Neymar) au Real Madrid ilivyowahi kuwa na BBC (Bale, Benzema na CR7), ni zamu ya Wananchi kutamba na MAP
Mpaka sasa utatu huu umechangia zaidi ya asilimia 70 ya mabao yaliyofungwa na Yanga kwenye michuano mbalimbali
Kwenye ligi kuu ya NBC, wachezaji hao wamepachika mabao tisa kila mmoja akiwa amefunga mabao matatu. Lakini pia wamechangia katika kupatikana kwa mabao mengine matano
Katika mchezo wa mwisho wa ligi dhidi ya Geita Gold kabla ya mapumziko ya FIFA, wote walifunga katika ushindi wa mabao 3-0

Takwimu zinaonyesha angalau mmoja anafunga bao katika kila mchezo ambao wanatumika
Mchezo unaofuata kwa Yanga baada ya mapumziko ya kalenda ya FIFA ni dhidi ya Azam Fc ukitarajiwa kupigwa Oktoba 22 katika uwanja wa Azam Complex
Mara ya mwisho Yanga na Azam Fc zilikutana kwenye Ngao ya Jamii, Aziz Ki akifunga katika ushindi wa mabao 2-0 katika uwanja wa Mkwakwani
Maxi alikuwepo uwanjani katika mchezo huo ambao Pacome hakupata nafasi ya kucheza, lakini pasipo shaka katika mchezo unaofuata wote watakuwepo