Mlinda lango namba moja wa Yanga Djigui Diarra ameendelea kujihakikishia nafasi kwenye kikosi cha Mali kuelekea michuano ya Afcon 2023 itakayofanyika Januari 2024 huko Ivory Coast
Jana Diarra alikaa langoni kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Uganda, wenyeji Mali wakiondoka na ushindi wa bao 1-0
Huo ulikuwa mchezo wa nne mfululizo Diarra anaanza kwenye kikosi cha kwanza cha Mali
Katika mchezo huo Diarra alikaa langoni kwa dakika zote 90 huku upande wa Uganda, Khalid Aucho akikabidhiwa kitambaa cha unahodha
Mali watacheza mechi nyingine ya kirafiki Oktoba 17 dhidi ya Saudi Arabia wakati Uganda wao watachuana na Zambia Oktoba 17
Diarra na Aucho ni miongoni mwa wachezaji 10 wa Yanga ambao wako kwenye majukumu ya timu za Taifa
Wachezaji wengine saba wako timu ya Taifa ya Tanzania wakati Stephane Aziz Ki yuko timu ya Taifa ya Burkina Faso
Walio kikosi cha Stars ambacho kesho Jumapili kitaumana na Sudan katika mchezo utakaopigwa Saudi Arabia ni Metacha Mnata, Nickson Kibabage, Dickson Job, Ibrahim Bacca, Bakari Nondo, Mudathir Yahya na Clement Mzize