Kipa Aigle Noir ajifua na Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Oct 2023
Kipa Aigle Noir ajifua na Yanga

Katika mazoezi ya Yanga yanayoendelea Avic Town kujiandaa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Azam Fc ambao umesogezwa nyuma kutoka Oktoba 25 mpaka Oktoba 22, kuna nyota mpya ameonekana

Ni mlinda lango Ndizeye Aime aliyeonekana katika viunga vya Avic Town wiki hii akijifua kwenye kikosi cha kocha Miguel Gamondi

Aime mwenye umri wa miaka 21, msimu uliopita aliitumikia Aigle Noir ya Burundi

Hata hivyo taarifa za uhakika ni kuwa mlinda lango huyo hajasajiliwa bali amepewa nafasi ya kufanya mazoezi na timu wakati huu wachezaji wengi wakiwa wameondoka kutimiza majukumu ya timu za Taifa

Yanga inawakosa wachezaji 10 ambao wanatekeleza majukumu ya timu za Taifa kwenye mechi za Kimataifa za kirafiki zilizo kwenye kalenda ya FIFA

Lakini hii inaweza kuwa fursa nzuri kwake kama ataweza kumshawishi Gamondi anaweza kumuweka kwenye orodha ya nyota wapya atakaowasajili

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’