Gamondi awatega nyota Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Oct 2023
Gamondi awatega nyota Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ameweka msimamo kwa wachezaji wake kuhakikisha wanajituma na kutumia vyema nafasi pale wanapopewa muda wa kucheza mechi

Pamoja na ubora ambao kikosi chake kimeonyesha katika mechi nyingi msimu huu, Gamondi hajafurahishwa na viwango vya baadhi ya wachezaji

Gamondi alikerwa na kiwango kilichoonyeshwa na nyota wake katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc, mchezo ambao Yanga ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1

Kocha huyo raia wa Argentina alifanya mazungumzo na baadhi ya wachezaji na kuweka msimamo wake dhidi ya wale ambao hawatatimiza majukumu yao vyema uwanjani

Katika moja ya mahojiano yake, Gamondi aliweka msimamo kuwa anahitaji wachezaji walio tayari kuipambania Yanga na kufikia malengo

"Kila mchezaji ana umuhimu ndani ya timu lakini nataka kuona wote wanakuwa sawa na kupambania malengo ambayo tumejiwekea kwa kadiri wawezavyo" 

"Yanga ni timu kubwa, kila mchezaji anapaswa kufahamu na ni lazima aonyeshe anastahili kuwa hapa," alisema Gamondi

Ni wazi Gamondi anajipanga kufanya maboresho zaidi kwenye usajili wa dirisha dogo ambao utafunguliwa Disemba 15

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
2h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
6h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
11h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
11h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
15h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’