Kiungo mshambuliaji wa Yanga Maxi Nzengeli amesema umoja na ushirikiano kutoka kwa viongozi, benchi la ufundi, wachezaji na mashabiki ni chachu katika kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali msimu huu
Chini ya Kocha Miguel Gamondi, Yanga inatajwa kuwa timu inayocheza kandanda safi zaidi la kushambulia, Wananchi wakitinga hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa baada ya kusubiri kwa miaka 25
"Kikubwa ni maandalizi na tunamshukuru Mwenye ez Mungu ambaye anatupa nguvu ya kufanya kazi wakati wote. Benchi la ufundi wanatupa mbinu ambazo zinatuandaa kwa ajili ya kupambana kila mechi. Viongozi nao wanahakikisha timu inakuwa kwenye mazingira mazuri wakati mashabiki wako nasi katika kila mechi tunazocheza"
"Naamini tukiendelea kushirikiana sote kwa pamoja, tunaweza kufanya vizuri sana msimu huu," alisema Maxi
Maxi ni miongoni mwa wachezaji walio katika kiwango bora sana katika kikosi cha Yanga
Amepachika jumla ya mabao matano na kutoa pasi nne za mabao katika mechi za mashindano yote
Maxi ni silaha muhimu ya Yanga kuelekea hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo Yanga iko kundi D ikiwa na Al Ahly, Madeama na CR Belouizdad
Mechi za makundi zitaanza kutimua vumbi Novemba 25 Yanga ikianzia ugenini dhidi ya CR Belouizdad