Yanga imeondoka na alama zote tatu katika uwanja wa CCM Kirumba baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Iliwachukua Yanga dakika 43 kuvunja ukuta wa Geita Gold waliokuwa wakizuia na watu 10, Pacome Zouzou akifunga bao kwa shuti kali baada ya pasi ya Yao Yao
Dakika mbili baadae Yanga ikaweka kambani bao la pili likifungwa na Stephane Aziz Ki aliyemalizia shambulizi alilolianzisha mwenyewe akimpasia Maxi Nzengeli ambaye nae akaurejesha mpira kwake ndani ya eneo la hatari na Aziz Ki kuujaza kimiani kwa mguu wake wa kulia
Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa na uongozi wa mabao 2-0. Kipindi cha pili Yanga ilirejea na kasi ileile na kufanikiwa kufunga bao la tatu kupitia Max baada kunyan'ganya mpira katika eneo la hatari la Geita Gold
Ni 'reaction' nzuri kutoka kwa wachezaji wa Yanga ambao wamerejesha furaha ya mashabiki wao baada ya ushindi huo
Yanga imesogea nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikifikisha alama 12, ikiendelea kuwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa



