Jeshi la Yanga liko kamili kazi kwako Lwandamina

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Mar 2018
Jeshi la Yanga liko kamili kazi kwako Lwandamina
Uongozi wa Yanga umethibitisha kuwa sasa hawana mchezaji majeruhi baada ya wachezaji wote waliokuwa wagonjwa kuanza mazoezi.

Donald Ngoma na Amissi Tambwe wamekamilisha idadi ya wachezaji wajeruhi waliorejea kikosini baada ya kumaliza program maalum zilizokuwa chini ya uangalizi wa daktari.

Hii ni habari njema kwa Yanga ambayo msimu huu utaingia katika historia yake kutokana na changamoto ya majeruhi kwa wachezaji wake tegemeo.

Kuna kipindi wachezaji 11 wa kikosi cha kwanza walikuwa nje wakiugua na kuwaachia vijana chipukizi kutekeleza ipasavyo majukumu ya kuipeleka Yanga mbele.

Huu ni msimu ambao benchi la Ufundi la Yanga linaloongozwa na kocha George Lwandamina limedhihirisha uborwa wake kwa kutengeneza kikosi imara kisichotegemea mchezaji mmoja mmoja.

Yanga hii ya sasa mchezaji yeyote anaweza kupangwa katika mchezo wowote na akafanya vizuri. Tumeliona hilo likifanyika mara nyingi msimu huu.

Yanga imeshinda michezo wakati mwingine bila ya kuwa na wachezaji waandamizi kama Andrew Vicent, Papi Tshishimbi, Obrey Chirwa, Thabani Kamusoko, Ibrahim Ajib, Donald Ngoma, Amissi Tambwe na wengineo.

Yanga ilikuwa timu pekee ambayo ilitumia vijana wengi chipukizi kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi mapema mwezi Januari mwaka huu na kutinga hatua ya nusu fainali.

Michuano hiyo ndio iliyowahakikishia namba Ramadhani Kabwili, Hamisi Kessy, Said Juma Makapu na Juma Mahadhi kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga.

Na ni baada ya michuano hiyo Yanga ilirejea kwenye ligi ikiwa na nguvu mpya na sasa ikiwa imeweka rekodi ya kushinda michezo tisa mfululizo.

Kurejea kwa wachezaji waliokuwa majeruhi ni jambo jema zaidi na bila shaka wataiongezea Yanga nguvu hasa ikizingatiwa inakabiliwa na michuano mitatu.

Sasa kocha George Lwandamina vijana wake wengi ni kama wamefuzu kuitumikia Yanga, anaweza akaamua kutumia vikosi tofauti kwenye michuano yote.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
9h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
14h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’