Baada ya kupoteza mchezo uliopita wa ligi kuu ya NBC, Yanga leo ina nafasi ya kujisahihisha itakapoikabili Geita Gold katika mchezo utakaopigwa uwanja wa CM Kirumba
Huu ni mchezo muhimu sana kwa Yanga kushinda ili kurudisha furaha ya mashabiki wao ambayo ilitibuliwa na kipigo cha Ihefu Fc
Hata hivyo hautakuwa mchezo rahisi Geita Gold haijawahi kuwa mpinzani mwepesi inapokutana na Yanga
Katika mchezo huo Yanga itakosa huduma ya wachezaji wake wawili mlinzi wa kati Ibrahim Bacca na Farid Mussa ambao wanachangamoto za kiafya
Kikosi cha Yanga jana kilipata nafasi ya kufanya mazoezi yake ya mwisho katika uwanja wa CCM Kirumba ari na morali ya wachezaji ikiwa juu
Ni wazi katika mchezo wa leo Wananchi watarajie kuiona ile Yanga yao waliyoishuhudia katika michezo ya nyuma kabla ya kukutana na Ihefu Fc
Mchezo utapigwa saa 10 jioni