Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema klabu inatarajiwa kuzindua jezi maalum ambazo zitatumika kuanzia hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Msimu uliopita Yanga iliingia makubaliano ya kampuni ya Haier kuwa wadhamini wakuu wa klabu kuanzia hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho (CAF CC) ambalo Yanga walifanikiwa kufika fainali
Kamwe ametamba kuwa jezi wanazokwenda kuzindua msimu huu zitakuwa bora zaidi ya zile za msimu uliopita
"Hivi karibuni tutazindua jezi zetu kwa ajili ya michuano ya Kimataifa. Niwaambie tu, tunakwenda kuzindua jezi bora zaidi ya zile tulizotumia msimu uliopita," alisema Kamwe
Kamwe alitoa kauli hiyo jana katika hafla maalum iliyoandaliwa na @yanga_on_fire_group, @yanga_friends_forever na @yanga_unbeaten_fans baada ya kutimiza mwaka mmoja katika majukumu ya uongozi kwenye kitengo cha habari na Mawasiliano
Aidha Kamwe amewataka Wanachama na Mashabiki wa Yanga kuendelea kuwa wamoja katika kuiunga mkono timu na kuhakikisha wale wenye vikundi wanajisajili kuwa Wanachama
Yanga imesajili zaidi ya Wanachama 40,000 katika kipindi cha mwaka mmoja, ambapo wale ambao hawajahuisha Uwanachama wao wametakiwa kulipia ada zao ili waendelee kuwa Wanachama hai