Mashabiki wa Yanga wana shauku kubwa ya kumuona winga wao fundi Skudu Makudubela aliyebarikiwa vitu vingi mguuni mwake
Tangu aitumikie Yanga kwa takribani dakika saba katika mchezo wa Ngao ya Jamii, Skudu alipata majeraha ambayo yalimuweka nje kwa takribani wiki tatu
Skudu amerejea kikosini baada ya kupona majeraha hayo na anachosubiri ni wito wa kocha Miguel Gamondi kumjumuisha katika kikosi chake
Fundi huyo wa mpira alikuwa benchi katika mchezo uliopita wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc uliomalizika kwa Yanga kushinda bao 1-0
Gamondi alitaja sababu ya kutomtumia katika mchezo dhidi ya Namungo Fc kuwa mchezo huo ulikuwa na presha kubwa na yeye ametoka katika majeraha
Pengine Wananchi watarajie kumuona kwenye mchezo dhidi ya Al Merrikh siku ya Jumamosi baada ya mchezaji huyo kuwa fit kwa asilimia 100
Skudu anashiriki kikamilifu mazoezi ya Yanga yakiwa ni maandalizi ya mchezo dhidi ya Al Merrikh