Mechi ya Jumamosi dhidi ya Al Merrikh ni mechi muhimu kwa Yanga ambao itaingia kwenye vitabu vya kumbukumbu vya mabingwa hao wa nchi
Ni mechi ambayo inaweza kuirudisha Yanga kwenye hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa baada ya takribani miaka 25 kupita
Ni bahati mbaya uwanja wa Benjamin Mkapa bado uko kwenye ukatabati hivyo ni mashabiki takribani 9,000 tu ambao watapata nafasi ya kuingia dimba la Azam Complex kushuhudia mchezo huo
Ni wazi zoezi la kukata tiketi litafungwa mapema hivyo Mwananchi unapaswa kukamata tiketi yako mapema usisubiri siku ya mchezo na wala usinunue tiketi uwanjani kuepuka matapeli
ADVERTISE HERE