Mechi ya pili ya Kimataifa nyumbani dhidi ya Al Merrikh inakwenda na Stephane Aziz Ki. Ni siku ambayo imepewa jina la 'Key Day'
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema msimu huu wamedhamiria kwenda hatua ya makundi ligi ya mabingwa na bahati nzuri wanayo funguo ambayo itawapeleka makundi
"Hatujacheza kwa muda mrefu hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa wakati huu tunakwenda na funguo tunayo"
"Siku ya Jumamosi ni siku maalum kwa Stephane Aziz Ki. Ni Key Day, tunataka kila Mwanayanga anayekuja uwanjani aje na pensi lake pamoja na fungua mkononi"
"Jumamosi ni Key Day, mtoko wetu ni 'njunga', jezi na funguo mkononi sote tutakutana Azam Complex," alitamba Kamwe
ADVERTISE HERE