Khalid Aucho 'The tank'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Sep 2023
Khalid Aucho 'The tank'

Katika kikosi cha Yanga Kocha Miguel Gamondi amekuwa na uhuru wa kufanya 'rotation' ya wachezaji kutoka mechi moja na nyingine kulingana na mahitaji ya mchezo husika

Hata hivyo kiungo Khalid Aucho anaweza kuwa moja ya wachezaji ambao Gamondi hafanyi kamali kumuweka nje

Katika msimu huu Aucho alikosa mechi moja tu ya mashindano dhidi ya Asas Fc ukiwa mchezo wa mkondo wa pili hatua ya awali ligi ya mabingwa

Unaweza kusema kama nyumba inahitaji msingi ili iweze kuwa imara basi Aucho yeye ndiye msingi wa Yanga katika eneo la kiungo

Aucho alijipambanua kuwa mchezaji muhimu tangu mabingwa hao wa nchi wakinolewa na Nasreddine Nabi

Ni wazi kukosekana kwake katika mechi mbili za fainali kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya USM Alger msimu uliopita kulikuwa na athari na pengine kama angekuwepo matokeo yangeweza kuwa tofauti

Umahiri wake katika eneo la kiungo unaipa Yanga utulivu na kucheza aina ya soka la kuvutia

Msimu huu yawezekana Aucho na Djigui Diarra ndio wachezaji waliocheza dakika nyingi zaidi kwenye kikosi cha Yanga mpaka sasa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
2h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
20h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’