Nahodha wa Yanga Bakari Mwamnyeto amesema dhamira ya wachezaji wote ni kuhakikisha wanashinda mchezo dhidi ya Al Merrikh na kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Jumamosi ijayo Septemba 30 2023 Yanga itakuwa na nafasi muhimu ya kutinga makundi na kumaliza ukame wa miaka 24 bila ya kucheza hatua hiyo Wananchi wakihitaji ushindi au matokeo yoyote ya sare baada ya kushinda mabao 2-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza
"Tunajua nia na matamanio ya mashabiki wetu ni kucheza hatua ya makundi sisi kama wachezaji tunawahakikishia tutamalizia kazi iliyobaki hapa nyumbani"
"Kule Rwanda sisi tulikuwa wageni lakini ni kama tulikuwa nyumbani sasa siku ya Jumamosi tunawaomba mashabiki wetu waje kwa wngi zaidi ya kile walichofanya Rwanda sisi tutapambana ili kuhakikisha tunawapa furaha," alisema Mwamnyeto
Mwamnyeto alikosa mchezo wa kwanza akipewa ruhusa na uongozi wa Yanga kwenda kumuuguza Baba yake aliyekuwa mgonjwa
Tayari amerejea na akijifua na wachezaji wenzake kujiandaa na mchezo dhidi ya Al Merrikh
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi alitoa mapumziko ya mwishoni mwa wiki na wachezaji watarejea mazoezini kesho Jumatatu