Inashangaza sana mijadala kutoka kwa wachambuzi huwa mingi pale wachezaji wa Simba wanapokumbana na changamoto za kuchezewa rafu katika mechi zao lakini hutaiona mijadala hiyo inapowatokea wachezaji wa timu nyingine ikiwemo Yanga
Ukweli ni kwamba matukio ya wachezaji kufanyiana rafu mbaya yanapaswa kukemewa na kila mtu bila ya kujali aliyefanyiwa anacheza timu ganii
Ni juzi tu mchezaji wa Yanga Joyce Lomalisa alichezewa rafu mbaya na Hashim Manyanya wa Namungo Fc, rafu iliyomfanya ashindwe kuendelea na mchezo katika kipindi cha pili
Suala la mwamuzi kutotoa kadi nyekundu ni mwendelezo wa aina ya matukio ya kushangaza ambayo waamuzi wetu hufanya katika ligi kuu Tanzania Bara 'Soka letu kivyetu vyetu'
Lakini hakukuwa na mijadala huko kwenye vipindi vya michezo kukemea tukio lile kama ilivyotokea kwa mchezaji Henock Inonga aliyeumizwa na Hija Ugando wa Coastal Union jana
Ni bahati zaidi kwa Yanga kwani imekumbana na matukio mengi ya aina hiyo mojawapo baya likimuhusisha Salum Abubakar akifanyiwa rafu mbaya na Inonga katika mchezo wa Ngao ya Jamii msimu uliopita
Nafikiri masuala yanayohusiana na afya za wachezaji hayapaswi kujadiliwa kishabiki, tukemee na kuchukua hatua kwa matukio yote na sio kuchagua matukio ya kukemea
Tunazungumza yanapowakumba wachezaji wa timu tunazozipenda na kukaa kimya pale wanapofanyiwa wachezaji wa timu nyingine, hii sio sawa