Kulingana na mtandao wa BIN ZUBEIRY, kiungo mshambuliaji wa Yanga Deus Kaseke amemalizana na Singida United ambapo kesho anatarajiwa kujiunga na kikosi cha timu hiyo jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo ameuthibitishia mtandao huo kuwa tayari wameshamsajili Kaseke.
"Kweli tumekwishafikia makubaliano naye (Kaseke), hivyo kesho ataungana na wenzake Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya," amesema.
Kaseke alikuwa bado hajaungana na wachezaji wa Yanga walioanza maandalizi ya msimu mpya wiki iliyopita pia alikuwa bado hajasaini mkataba mpya licha ya mazungumzo kufanyika.
Kaseke anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa kutoka Yanga na Singida United baada ya timu hiyo kumsajili mlinda lango Ali Mustafa 'Barthez' juzi.

ADVERTISE HERE