Yao anaendeleza ubora wake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Sep 2023
Yao anaendeleza ubora wake

Mlinzi wa kulia wa Yanga Yao Kouassi ameendelea kuonyesha thamani yake katika kikosi cha Yanga jana akitoa pasi ya bao pekee lililofungwa katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc uliopigwa uwanja wa Azam Complex

Katika mechi tatu ambazo Yanga wamecheza kwenye ligi mpaka sasa, Yao amechangia mabao matatu, akifunga bao moja na kutoa pasi mbili za mabao

Nyota huyo amekuwa chanzo cha mashambulizi mengi ya Yanga yanayopita upande wa kulia

Yao na Jesus Moloko ndio vinara wa kutoa pasi za mabao kila mmoja akiwa ametoa pasi mbili

Wachezaji wengine waliohusika kutoa pasi moja ya bao ni Hafiz Konkoni, Nickson Kibabage, Dickson Job, Stephane Aziz Ki na Maxi Nzengeli

Aidha Mudathir Yahya, Aziz Ki na Maxi ndio vinara wa mabao kila mmoja akiwa amepachika mabao mawili wakati Pacome Zouzoua, Konkoni, Job, Yao na Musonda kila mmoja amefunga bao moja

Yanga imepachika mabao 11 kwenye ligi msimu huu pasipo kuruhusu bao lolote kutikisa nyavu zake katika michezo mitatu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’